Kenyan music lyrics

  • fnt+
  • fnt=
  • fnt-

John

John

(0 votes, average 0 out of 5)

LISTEN TO 'JOHN'

Artist: Wakimbizi
Song: John
Album: Raha
Producer: DJ Stone

Verse 1 (Mariko)

mimi ni Dokta Mark kutoka kwa wakoloni
ninashangazwa sana na huu jamaa anaitwa Johnny
ametenda madhara na washikaji hawaoni
bado wanafurahia Johnny kumtia machoni
ameongeza idadi kibao tu ya magonjwa
na bado wanamsifu eti Johnny ni mtu poa
najaribu kujiuliza maswali sipati jibu
mbona humpendi mchana wanampenda tu usiku
kama mchana hana nguvu ana nguvu tu usiku
Johnny, Johnny kweli wee ni mpita njia
iwe mzee ama kijana bado Johnny ataingia
mradi tu mwenzie kipofu aonyeshwe njia
ata map nimwibie mwenzie hatapotea
wanampenda Johnny na Johnny anawapenda
John tunakusifia at yahoo.com
nyumba zote mtakwenda lakini Johnny ndio boss

Chorus
John, nampenda John
ni kipofu jamani wala tena ye haoni
John, nampenda John
ni bubu kiziwi anayeishi msituni
John, nampenda John
swali ninauliza mnampendea nini
John, nampenda John

Verse 2 (Andre)


Andre wa Wakimbizi anashangazwa na huyu John
watu wa jinsia moja wanampenda sana John
tena la ajabu sana Johnny si handsome
ana jicho moja tu ndogo kama can
lakini wanampenda hata kuliko chakula
wengine wakimkosa ndani ya nyumba wananuna
wengi wanavaa vizuri ili wampendeze John
na hilo jicho lake kawaida halioni
wengine wanampenda akiwa moto ameshika
wengine wanafurahia akiwa amekasirika
idadi kubwa yao wanapenda akitapika
ni hoji waliomwona walisema hana mikono
shughuli anafanyaje kama ye hana mikono
kina Beyonce
kina Ashanti
wote wanalia na John
hata Talia wa Kenya analia na John
na John ni cartoon anayeishi msituni

Chorus
John, nampenda John
ni kipofu jamani wala tena ye haoni
John, nampenda John
ni bubu kiziwi anayeishi msituni
John, nampenda John
swali ninauliza mnampendea nini
John, nampenda John

Verse 3 (Andre)
Johnny anapenda raha
Johnny hapendi kadhaa
na hiyo ndio sababu msituni amezubaa
Johnny huvaa sweater weather ikiwa rainy
tena si sweater ovyo yake iko specially
ambayo huivaa siku yake officially
Johnny hafungi tie lakini ye hujidai
tena hakunywi chai anadai kwake hakufai
ukija kumsabai cheki ana-feel shy
akiona anawapenda Johnny ana-feel high
Johnny haeleweki mara amekwenda kazini
mara amekasirika amekwenda zake mwezini
sasa atarudi lini
wengi wanamngoja chini
maskini matajiri wote wanamngoja chini
Johnny hawabagui wote anawapa vinywaji
ukija na container Johnny atakupa kinywaji

Chorus
John, nampenda John
ni kipofu jamani wala tena ye haoni
John, nampenda John
ni bubu kiziwi anayeishi msituni
John, nampenda John
swali ninauliza mnampendea nini
John, nampenda John



Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Digg! Reddit! Del.icio.us! Google! Live! Facebook! StumbleUpon! MySpace! Twitter!
Comments
Add New
+/-
Write comment
Name:
Email:
 
Website:
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
Security Image
Please input the anti-spam code that you can read in the image.
 
KenyanLyrics.com


Follow KenyanLyrics on Twitter